Mtoto wa pili wa Princess Diana, Prince Harry wa Uingereza amesema kuwa alitafuta ushauri nasaha miaka minne iliyopita kukabiliana na huzuni ya kumpoteza mama yake mzazi.

Harry amesema kumpoteza mama yake katika umri mdogo kulisababisha aishi maisha ya hovyo.

Prince Harry amesema alitafuta ushauri wa kitaalamu akiwa na miaka 28 baada ya kupitia miaka miwili ya vurugu.

Princess Diana alifariki kwa ajali ya gari mjini Paris August 31, 1997. Kifo chake kilisababisha mshtuko mkubwa na kuiweka Uingereza katika kipindi kirefu cha maombolezo.

Akijulikana na kama princess wa watu, Diana alifunga ndoa na Prince Charles kwenye harusi ya kifahari katika kanisa la St. Paul mjini London mwaka 1981.

Alimzaa mwanae wa kwanza William mwaka 1982, na wa pili, Harry, 1984 ambapo alikuwa na watoto wawili tu.

Harry alipata shida kukabiliana na macho ya vyombo vya habari. Miaka mitano baada ya kifo cha mama yake, akiwa na miaka 16, baba yake alimpeleka rehab, siku moja baada ya kukiri kunywa sana pombe na kuvuta bangi.

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *