Naibu waziri wa Afya, Mandeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamis Kigwangalla amesema kuwa serikali inatarajia kupigwa marufuku utengenezaji na uingizaji wa pombe aina ya viroba ndani ya miezi mitatu ijayo.

Dkt. Kigwangalla amesema hayo Bungeni wakati akijibu hoja za wabunge waliokuwa wakilalamikia kilevi hicho kinachopunguza nguvu kazi ya taifa.

Naibu Waziri huyo amesema kuwa baada ya miezi mitatu kilevi hicho kitapigwa marufuku kutengenezwa au kuingizwa nchini pamoja na kuzipa mianya yote ya uingizaji wa kilevi hicho ambacho hutumiwa na vijana wengi.

Kwa upande wake Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko amesema kuwa pombe hizo husababisha vifo kwa vijana wengi kutokana na matumizi ya pombe hiyo hivyo kupelekea kupunguza nguvu kazi ya taifa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *