Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga limeuzingira mgodi wa Bulyanhulu baada ya mkuu wa mkoa wa Shinyanga, Zainab Tellaack kuzuiwa kuingia ndani ya mgodi huo.

Mkuu wa mkoa huyo alikwenda kukagua iwapo uzalishaji unaendelea bila kuwepo maofisa wa Wakala wa Ukaguzi wa madini nchini (TMAA).

Jeshi hilo la Polisi limefanya hivyo baada ya mkuu wa mkoa huyo kuagiza kuimarisha ulinzi eneo lote la mgodi na kuhakikisha hakuna mtu anayeingia wala kutoka ndani ya mgodi huo.

Mkuu wa mkoa huyo pia alitembelea mgodi wa Buzwagi ambao pia unamilikiwa na kampuni ya Acacia kama ulivyo mgodi wa Bulyanhulu.

RC Tellaack na msafara wake waliruhusiwa kuingia ndani ya mgodi wa Buzwagi na kukagua uzalisha unavyoendelea na kukuta uzalishaji umesitishwa kwenye mgodi huo kutokana na kukosekana kwa maofisa wa TMAA.

Maofisa wa TMAA waliondoka baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kuivunja bodi hiyo na kuwatimua wakaurugenzi wa TMAA.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *