Mkurugenzi wa Upelelezi na Makosa ya Jinai (DCI), Kamishna Robert Boaz amesema kuwa ofisi yake imetoa taarifa kwa kutumia mfumo wa kiuchunguzi wa Jeshi la Polisi la kimataifa (Interpol) kumsaka mwanachama wa Chadema, Ben Saanane aliyepotea toka mwaka jana.
Ben Saanane anadaiwa kupotea katika mazingira ya kutatanisha na hajawahi kuonekana toka Novemba mwaka jana hadi sasa ni miezi mitano.
Kamishana Boaz amesema kuwa licha ya kupokea taarifa tofauti kuhusu mwanachama huyo lakini hakuna hata mwanga wa kusaidia kupatika kwake.
Kamishna huyo amesema kuwa wamewahoji watu wote ambao walikuwa nae karibu kabla ya kupotea kwake lakini hakuna mafanikio.
Pia amesema kuwa wamewahoji watu waliokuwa wanaongelea suala hilo katika vyombo vya habari pamoja na majukwaa mbali mbali lakini hakuna mafanikio.
Kwa mujibu wa mwanasheria mkuu wa Chadema, Tundu Lissu alisema kuwa Saanane mara ya mwisho kuwasiliana na Mbowe ilikuwa Novemba 14 mwaka jana baada ya hapo hapakuwa tena na mawasiliano na kiongozi huyo.