Jeshi la Polisi nchini limewasimamisha kazi maofisa 12 wa polisi ambao ni miongoni mwa wale waliotajwa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda wanaojiuhusisha na uuzaji wa madawa ya kulevya.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu amewaambia wanahabari katika makao makuu ya Polisi huku akisema kuwa Polisi ndiyo chombo kinachoongoza mapambano juu ya madawa hayo huku akisema kuwa hatua zitachukuliwa dhidi ya askari atakayetuhumiwa.

polisi12

Pia amesema kuwa uchunguzi unaendelea dhidi ya idadi kubwa ya wasanii ambao pia walitajwa na Makonda na kuripoti katika vituo vya polisi ili kuhojiwa.

IGP Mangu amesema kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya maafisa hao 12 uchunguzi utakapokamilika.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Dar es Salaam Simon Sirro amesema operesheni ya kuwakamata watu hao ilianza tangu Ijumaa ambapo watu watano walitiwa lupango na kufikisha idadi ya watu waliokamatwa hadi leo kufikia 17.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *