Katibu wa Itikadi na Uenezi (CCM), Humphrey Polepole ameiagiza Serikali kupeleka chakula Wilayani Longido Mkoani Arusha ili kukabiliana tatizo la upungufu wa chakula Wilayani humo.

Polepole amesema hayo alipokuwa Longido katika mkutano wa CCM na kusema serikali italeta tani 500 za chakula hicho siku ya Jumatatu kwa awamu ya kwanza na kusema chakula hicho kitauzwa kwa kilo moja kati ya shilingi mia tano mpaka mia sita.

Amesema kuwa tani mia tano kutoka Jumatatu zitafika Longido na kilo moja itauzwa kwa mia tano mpaka mia sita ikiwa ni awamu ya kwanza.

Polepole amesema kuwa anataka kuona suala la gunia kuuzwa laki moja na hamsini linamalizika kwani jambo hilo haliwezekani.

Pia amesema kuwa atakaye zuia chakula hicho kisifike wilayani humo iwe serikali au kwenye chama huyo mtu tutakula atashughulikiwa maana anatutenga serikali ya Chama Cha Mapinduzi na wananchi.

Mbali na hilo Polepole aliweka wazi kuwa hakuna Chama kama chama cha Mapinduzi kwani wao wanatatua matatizo ya wananchi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *