Kiungo wa Manchester United, Paul Pogba hatokuwepo kwenye kikosi cha klabu hiyo kitakachocheza dhidi ya Middlesbrough kwenye mechi ya ligi kuu nchini Uingereza siku ya Jumapili baada ya kuumia misuli.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa aliumia kipindi cha pili cha mechi ya ligi ndogo ya klabu Ulaya, Europa League, kati ya United na FC Rostov ya Urusi na ikamlazimu kuondoka uwanjani.

Manchester United walishinda 1-0 kupitia bado la Juan Mata na wakasonga hati robofainali kwa ushindi wa jumla wa 2-1 dhidi ya Rostov.

Pogba mwenye umri wa miaka 24, pia anatarajiwa kukosa pia mechi za timu ya taifa ya Ufaransa dhidi ya Luxembourg na Uhispania baadaye mwezi huu.

Kocha wa Manchester Unitd, Jose Mourinho hakusema Pogba anatarajiwa kukaa nje muda gani kutokana na majeraha hayo.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *