Kiungo mshambuliaji wa Manchester United, Paul Pogba ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa kombe la Europa ligi baada ya kuisadia timu hiyo kutwaa ubingwa huo msimu uliopita.
Mchezaji huyo amepwa tuzo hiyo leo jijini Monaco nchini Ufaransa baada ya kuchaguliwa na waandishi wa habari, makocha wa timu zilizoingia kwenye hatua ya makundi kombe hilo.
Wachezaji wenzake Henrikh Mkhitaryan na Zlatan Ibrahimovic pia walikuwemo kwenye kinyang’anyiro hicho kutokana na mchango wao baada ya Manchester United kutwaa ubingwa nchini Sweden dhidi ya Ajax.
Pogba alianza kwenye mechi zote 15 za Manchester United kwenye mashindano hayo mpaka mechi ya mwisho ya fainali ambapo walishinda 2-0 dhidi ya Ajax.
Wachezaji wengine waliochaguliwa kwenye kinyang’anyiro hicho ni Sergio Romero, Antonio Valencia, Eric Bailly, Daley Blind, Herrera, Mkhitaryan and Ibrahimovic.