Mshambuliaji wa Ujerumani, Lukas Podolski ametangaza kustaafu soka la kimataifa baada ya kuitumikia timu hiyo kwa miaka 12.

Mchezaji huyo alianza kuichezea timu ya taifa ya Ujerumani toka mwaka 2004 alipoitwa kucheza kwenye mechi yake ya kwanza dhidi Hangari mwaka huo

Lucas Podolski ni miongoni mwa wachezaji walioisaidia timu ya taifa ya Ujerumani kushinda taji la kombe la dunia mwaka 2014 nchini Brazil ambapo timu hiyo ilitwaa kombe hilo kwa kuifunga Argentina kwenye fainali.

Lukas+Podolski+Germany+v+Argentina+DM8ijthMPXtl

Podolski ambaye ni mzaliwa wa Poland ameichezea Ujerumani mechi 129 na kufunga jumla ya magoli 48 akiwa na timu hiyo.

Mchezaji huyo ambaye kwasasa anachezea klabu ya Galatasaray pia aliwahi kuzichezea klabu kama FC Koln, Bayern Munich na Arsenal amewaandikia ujumbe mashabiki wake baada ya kutangaza kustaafu soka la kimataifa kwa kuandika,”It was amazing, it was great, and it was an honour.”

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *