Kocha wa Yanga, Hans van Der Pluijm amesema kuwa imetosha vita ya maneno inayoendelea kati yao na Simba huku akisistiza kinachofuata atawanyamazisha wapinzani kwenye mechi yao hiyo.

Pluijm ameeleza zaidi kuwa wakati mwingine haifai kuongea maneno mengi kuelekea katika mchezo huo kwa kuwa kikosi chake kinafahamu nini cha kufanya ili kunyamazisha maneno yote yanayoendelea mitaani kuanzia kwa mashabiki, wapenzi, wadau mpaka viongozi.

Kocha huyo amesema “Huu mchezo umewaweka wengi kwenye presha, sasa sitaki kuongea sana, kuna maneno mengi yameshaongelewa na hii ni kwa kuwa ni mchezo wenye presha kwa sababu ni moja ya utani wa jadi uliopo, sasa kwa upande wetu nadhani hatuhitaji kuongea zaidi ya kufanya kazi hiyo Jumamosi.

Pia aliongezza kwa kusema “Wachezaji wangu wanafahamu mashabiki wanataka nini na nini cha kufanya kuzima hii presha iliyopo kwa mashabiki na wapenzi wengi wa Yanga, kumeshakuwa na maneno mengi lakini sasa ni vizuri kukaa kimya.

Simba na Yanga zinatarajiwa kumenyana kwenye mechi ya ligi kuu Tanzania bara itakayofanyika katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam siku ya jumamosi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *