Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Peter Msechu amekanusha habari zilizosambaa katika mitandao ya kijamii kuwa ameachana na mpenzi wake wa siku nyingi ‘Mama Lolo’.
Peter Msechu amesema kuwa taarifa hizo hazina ukweli wowote miongoni mwao kwani wapo pamoja kama zamani na hakuna tatizo lolote kati yao.
Peter Msechu amesema kuwa watu waliazna kuongea na yeye akaamua kuwachomekea huko ili kuwafurahisha na roho zao kwa sababu watanzania wanapenda kuona watu wakiharibikiwa na ndio maana aliamua kuwapima ili aone wanasema nini.
Pia amesema kuwa kwa jinsi walipotoka na Mama Lolo hawezi kumuacha hata mara moja kwa sababu wametoka mabli pindi hata hajawa msanii.
Habari za kauchana wawili hao zilisambaa katika mitandao ya kijamii mpaka kupelekea mashabiki kuanza kujiuliza ni kweli au maneno tu mitandaoni.