Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Marioo na Mimi Mars wamedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi, lakini wawili hao wamekuwa wakikanusha habari hizo.
Baada ya tukio la ugawaji wa tuzo za muziki wiki iliyopita ambapo Marioo alishinda tuzo mbili, wawili hao walikuwa pamoja wakisherekea na video zipo zikimuonesha Mimi Mars akiwa amelala na tuzo.
Hata hivyo, wikiendi iliyopita ndipo mambo yakawakolea, wakajikuta wakijirekodi video na kusambaa mitandaoni wakiwa ufukweni asubuhi asubuhi hivyo kama kuna aliyekuwa anabisha, basi aendelee kubisha.
Marioo na Mimi Mars ni wasanii wazuri, lakini tatizo nyota tu ambayo sasa wameamua kuisafisha.
Baadhi ya wataalam wanasema kuwa na kipaji tu haitoshi bali msanii anahitaji kujibrand kwa kuongeza jitihada nyingine binafsi.
Hicho ndicho walichogundua Marioo na Mimi Mars ambaye mbali na kuwa msanii wa muziki, pia ni mwigizaji mkali; kama huamini mtazame kwenye Tamthiliya ya Juakali anakotumia jina la Maria.
Kama penzi lao litakamata vichwa vya habari, watarajie sasa kuona sanaa yao inafika mbali na madili makubwa yakiwafuata kutokana na ufuatiliwaji mkubwa.