Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kwamba Serikali ina mpango wa kuanzisha usafiri wa majini ambao utakuwa ukianzia Posta mpaka Mbagala.
Usafiri huo mpya wa Boti za kisasa utasaidia kupunguza foleni za barabarani kwa wakazi wa Dar es Salaam.
Mkuu wa mkoa huyo amesema kwamba wanao mpango wa kuhakikisha kwamba wananchi wanaoishi Mbagala wanaanza kutumia usafiri wa boti badala ya usafiri wa Daladala.
Paul Makonda amesema tayari wameshatuma watu wanafanya upembuzi yakinifu kama inawezekana kutumia boti za kisasa kupunguza foleni za barabarani ndani ya Dar es Salaam.