Mwanamuziki wa dansi nchini, Papii Kocha amefunguka na kusema kuwa hataki kukumbuka matatizo yaliopita badala yake kwasasa anaangalia mambo ya mbeleni zaidi.
Papii Kocha amesema kuwa kwa sasa anaamua kupiga kazi tu kwani tayari ameshatengeneza nyimbo tatu ambazo tayari ameachia moja inayokwenda kwa jina la Waambie.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa hataki kabisa kufikria yaliyopita kwasababu yashatokea hivyo anaangalia Zaidi mambo yajayo.
Papii ameongeza kuwa, mashabiki wake wajitokeze Machi 10, mwaka huu kwenye Ukumbi wa King Solomon, Namanga, Dar wapate ladha halisi waliyoikosa kwa muda mrefu.
Papii Kocha na Babab yake mzazi, Nguza Viking walihukumiwa maisha jela kutokana na kosa la kunajisi watoto ambapo kwasasa wapo huru kwa msamaha wa rais Magufuli.