Kundi la muziki maarufu kutoka nchini Nigeria P-Square limegawanyika tena baada ya kupatanisha hap awali.

Kundi hilo lililofanya kazi kwa zaidi ya miaka mitano ambalo linawaunganisha ndugu wawili Peter na Paul Okoye linadaiwa kuvunjika rasmi baada ya wawili hao kuingia katika mgogoro mpya.

Kutokana na mgogoro huo Peter amemtuma mwanasheria wake Festus Keyamo kwa ajili ya kuweka makubaliano ya kundi na tayari ameashafanya hivyo.

Peter amekuwa akimshawishi kaka yake Paul wafanye kazi lakini kaka yake huyo ameonyesha kutokuwa na ushirikiano pia Paul alikatisha safari za muziki wa kundi Marekani bila ya kumshirikisha.

Kwa upande wa Paul yeye amekuwa akiwatumia familia yake katika mitandao ya kijamii kwa madai kuwa wekuwa wakipokea ujumbe wenye vitisho kutoka kwa Peter.

Pia taarifa zinasema kuwa meneja kundi hilo amabye ni kaka yao Jude Okoye aliwahi kumtishia kumpiga bastola Lola ambaye ni mke wa Peter.

Peter yeye amesema imetosha na hawezi kuendelea kufanya kazi sehemu kama hiyo hivyo ameamua kufanya kazi mwenyewe kama Mr P.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *