Mtayarishaji wa Bongo Fleva, P Funk Majani amesema mambo yanayoendelea kuyafanya mtoto wake pamoja na mzazi mwenzake Kajala yanaidharirisha familia yake.

 

Haya yamekuja baada ya kusambaa kwa video zikimwonyesha Paula akiwa kwenye pozi za kimahaba na msanii wa WCB, Rayvanny lakini baadaye tena kukaibuka picha mitandaoni na chatting zinazodaiwa kuwa ni za msanii Harmonize akimtongoza Paula licha ya kuwa na uhusiano wa kimapenzi na mama wa binti huyo ambaye ni Kajala.

 

P Funk amesema kuwa “Nilishawaambia tangu mwaka jana kwamba Mimi nilishajitoa, nilishanyoosha mikono kwa Paula, mtoto anatafuta laana alishaniambia wewe sio Baba yangu, Kajala sio familia yangu nilifanya uamuzi mbaya kuzaa na mtu ambaye sio sahihi kuwa mama, yanayoendelea hayanihusu.

 

 “Mimi kwa sasa nina familia yangu kama Baba na wanavyoendelea kufanya vinaathiri mpaka familia yangu hii nyingine kwa sababu inahusishwa nao, uchafu wao”.

 

Pia amesema kuwa “Maisha sio Instagram, vitu vya Kifamilia mnatatua Kifamilia naona Instagram wanasema ‘toa tamko’, nitoe tamko Instagram”.

 

Mwisho amemalizia kwa kusema kuwa Masuala ya kuvujisha mavideo sio sahihi, ugomvi wa kimapenzi kwa nini muweke mtandaoni, matatizo ya Familia huweki mtandaoni, jiheshimu utaheshimiwa,”.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *