Mwanamuziki nyota wa hip hop nchini Marekani, P. Diddy anatarajia kulipia zaidi milioni 40 kwa ajili ya mchoro mpya wa sura ya Notorious B.I.G.
Staa huyo alikuwa mjini Miami wiki hii kwenye onyesha la Sana Art Basel na kuitamani picha ya Notorious B.I.G. iliyokuwa ikiuzwa kwa kiasi cha dola elfu 20 zakimarekani.
Mchoro huu uliofanywa na msanii kutoka mitaa ya Miami Zeem Rock ulikuwa pembeni ya mchoro mwingine wa 2 Pac aliofanya yeye pia ila Diddy aliupenda zaidi wa Notorious B.I.G.
Mkali huyo ni miongoni mwa wasanii waliowahi kufanya kazi na mwanamuziki huyo B.I.G enzi za uhai wake ameamua kufanya hivyo kama ishara ya kumkumbuka.