Kiungo wa kati wa Arsenal Alex Oxlade Chamberlain amekataa uhamisho wa Chelsea baada ya klabu hiyo kukubali dau la £40m.

Oxlade Chamberlain anaamini kwamba Chelsea ilipanga kumtumia kama beki wa kulia huku lengo lake kuu la kutaka kutoka Arsenal likiwa hatua ya kuchezeshwa katikati.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa anataka kuelekea Liverpool.

Ombi kutoka Liverpool linatarajiwa kabla ya kukamilika kwa siku ya mwisho ya uhamisho Alhamisi ijapokuwa huenda kitita atakachonunuliwa kikawa chini ya kile ambacho Chelsea wanataka kutoa.

Iwapo hakutakuwa na makubaliano Oxlade Chamberlain yuko tayari kukamilisha mwaka wake wa mwisho wa kandarasi yake msimu huu kabla ya kuondoka kama mchezaji huru msimu ujao.

Arsenal wanataka makubaliano yoyote ya mchezaji huyo kuafikiwa haraka iwezekanavyo.

Oxlade Chamberlain ameanza kila mechi za Arsenal msimu huu ikiwemo kichapo cha siku ya Jumapili cha 4-0 dhidi ya Liverpool, ambapo alitolewa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *