Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amefanikiwa kushinda tuzo ya mwanamitando bora wa kiume katika maonyesho ya Swahili Fashion.
Baada ya kushinda tuzo hiyo mwanamuziki huyo amewashukuru mashabiki wake waliomuwezesha kwa kumpigia kura mpaka kushinda tuzo hiyo.
Msanii huyo amepewa tuzo hiyo na muandaaji wa Swahili fashion, Mustapha Hassanali katika ukumbi wa Serena Hotel jijini Dar es Salaam.
Tuzo hiyo ya Men Stylish Personality ya mwaka 2021 ilikuwa inagombaniwa na mastaa kadhaa wakiwemo muigizaji Rammy Galis, Rich Mitindo, Jimmy Chansa, Quick Rocka, Maxi Rioba na Jamal April.