Msanii wa Bongo Fleva, Ommy Dimpoz amesema kuwa alipokuwa kwenye matibabu nchini Ujerumani alikata tamaa ya kuishi kutokana na ugonjwa uliokuwa unamsumbua.
Ommy Dimpoz amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya koo kwa muda mrefu baada ya kusemekana kula chakula chenye sumu, hali ambayo ilimfanya afanyiwe upasuaji Afrika Kusini.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Nilifanyiwa operesheni kwa masaa manane, na nilipofika Ujerumani nilifanyiwa upasuaji na madaktari wa kijerumani wengi zaidi ukilinganisha na Afrika Kusini”.
Pia amesema kuwa “Nilipokuwa Ujerumani niliona wagonjwa wawili wakiwa wamekufa kwahiyo kupona kwangu ilikuwa ni mipango ya Mungu”.
Ameongeza kuwa “Nachoweza kusema kwa mtu kama Steve yeye ana namba yangu, lakini sijawahi kupata meseji ya pole unaendeleaje lakini nashangaa alipotoa kauli kwamba najua Ommy hawezi kuimba, kwa hiyo mtu anapokuwa na matatizo tusitumie hiyo advantage kwani hujui unayemuongelea ataipokeaje”.
Katika kuelezea shukrani zake kwa Mungu, mashabiki na watu wake wa karibu katika kipindi chote alichopitia, ameamua kutunga wimbo maalum unaoitwa ‘Ni wewe’ ambao tayari ameshauachia jana Februari 4.