Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi amefunguka na kusema kuwa lazima awafunge Yanga kwenye mechi ya Ngao ya Hisani itakayofanyika kesho katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Okwi ameeleza hayo kupitia mahojiano maalum aliyofanya na klabu yake na kusema hawezi kusema ni magoli mangapi atawapachika ‘gongo wazi’ Yanga kwa kuwa ni klabu ambayo anaiheshimu.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Uganda amesema kuwa  game ya Simba na Yanga siku zote inakuwa ngumu na haiwi raisi kama watu wanavyofikiria lakini atahakikisha anashinda goli kwenye mechi hiyo.

Pia Okwi aliendelea kwa kusema “nitahakikisha timu yangu inashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu ili tuweze kutoka na matokeo mazuri katika mchezo huo. Siwezi kusema tutawafunga magoli mangapi kwa kuwa ni timu ambayo ninaiheshimu lakini sisi tutajipanga kuhakikisha tunatoka na matokeo mazuri”.

Okwi ameanza kujitamba ikiwa imebakia siku moja kuchezwa kwa mechi ya watani wa jadi hapoa kesho ambapo mchezo huo umekuwa ukisubiliwa na watu mbalimbali waweze kujua ni nani siku hiyo ataweza kumfunika mwenzake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *