Aliyekuwa mgombea urais wa Kenya kupitia muungano wa NASA, Raila Odinga leo anatarajia kufichua ushahidi jinsi alivyoibiwa kura zake wakati wa uchaguzi nchini Kenya.
Odinga ambaye alikuwa akiwania urais kwa mara ya nne pia alibaini kwamba hatowania tena urais na kwamba aliwataka Wakenya kujua kilichofanyika wakati wa uchaguzi huo.
Odinga amedai kwamba wadukuzi waliingilia kompyuta za tume ya Uchaguzi na kuweka hesabu ambazo zilimpatia ushindi rais Uhuru Kenyatta.
Kiongozi huyo mkongwe wa upinzani nchini Kenya amesema kuwa “Sio swala la kuwa mbifansi, Sio suala kuhusu Raila Odinga, Sitawania urais tena ila tunataka Wakenya kujua kile kilichofanyika, na kile ambacho ulimwengu haujui kinafanyika.
Siku ya Jumapili Odinga aliwataka wafuasi wake kugomea kwenda kazini kutokana na kuibiwa kura zao kwenye uchaguzi mkuu wa nchi hiyo uliofanyika wiki iliyopita.
Tume ya taifa ya uchaguzi ya Kenya IEBF ilimtangaza Uhuru Kenyatta kuwa mshindi wa uchaguzi kwa muhula wa pili.