Mshambuliaji wa Yanga kutoka Zambia, Obrey Chirwa amepelekwa kwa mkopo katika klabu ya Plutnum nchini Zimbabwe.
Taarifa kutoka ndani ya klabu Yanga imesema kuwa makubaliano hayo yalifikiwa dakika chache kabla ya dirisha dogo la usajili kufungwa usiku wa saa 5:59 siku ya jana.
Taarifa hizo zimebainisha kuwa klabu hiyo imemsajili straika kutoka katika klabu ya Zesco, anayefahamika kwa jina Winston Kalengo kama mbadala wa Chirwa.
Kwa mujibu wa makubaliano katika mkopo huo, Yanga itakuwa ikimlipa Chirwa nusu mshahara, na nusu nyingine itakuwa ikilipwa na Platinum.
Chirwa ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa kwa kishindo katika klabu hiyo, ikidaiwa kuwa ndiye aliyekuwa mchezaji ghali zaidi akisajiliwa kwa dau la shilingi za kitanzania milioni 240, lakini hakuwa na mwanzo mzuri katika ligi kuu Tanzania Bara licha ya kuanza kufunga katika michezo ya mwisho ya mzunguko wa kwanza.