Rais wa zamani wa Marekani, Barack Obama amesema kuwa hakuweza kuzuia machozi yake alipomfikisha mwanawe mkubwa Malia katika chuo kikuu cha Harvard.

Obama amesema kuwa ilikuwa kama ”upasuaiji uliofanyika hadharani”, rais huyo wa zamani alizungumzia kuhusu wakati alipomfikisha Malia katika chuo kikuu cha Harvard.

Pia amesema kuwa Obama alielezea wakati huo siku ya Jumatatu wakati wa hafla ya wakfu wa Beau Biden. Shirika hilo la kusaidia jamii lilianzisha kwa heshima ya mwana{marehemu} wa aliyekuwa makamu wa rais Joe Biden

Obama amesema kuwa ”Mwisho wa maisha yetu chochote kile ambacho utakuwa umefanikiwa, ambayo tutayakumbuka ni maisha mazuri ya wana wetu na baadaye kile kitakacholetwa na wajukuu zetu”.

Malia mwenye umri wa miaka 19 aliamua kujiunga na chuo kikuu cha Harvard baada ya kupumzika kwa mwaka mmoja baada ya kukamilisha elimu ya shule za sekondari.

Obama mara kwa mara amekuwa akizungumza kuhusu umuhimu wa kuwa baba kwa wanawe.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *