Rais wa Marekani, Barack Obama amewahakikishia washirika wa Marekani kwamba Donald Trump ataendeleza heshima na ushirikiano wa kimataifa baina ya nchi yake nao wakati yeye atakapokabidhi urais mwezi Januari.

Obama ameyasema hayo wakati alipokuwa na mkutano mkubwa na waandishi wa habari .

Rais Obama amesema kwamba Donald Trump ameonesha nia ya kutaka kudumisha uhusiano baina ya Marekani na shirika la nyuklia duniani NATO.

Obama amesema kwamba Marekani lazima iendelee kuwa nguzo ya nguvu na nguzo ya matumaini kwa watu duniani kote.

Pia Obama ameongeza kusema kwamba uhusiano baina ya nchi na nchi unakwenda mbali zaidi ya nafasi ya urais na wanadiplomasia, majeshi na kwamba wakuu wenye hekima na busara wataendelea kuonesha ushirikiano na wenzao wanaoshughulikia masuala ya kigeni.

Obama alikuwa akizungumza kuelekea mwishoni mwa safari zake za mataifa ya kigeni akiwa mwishoni mwa madaraka yake ya urais.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *