Nyumba za mfanyabiashara, Said Lugumi zimeshindikana kununuliwa leo kwenye mnada uliopangwa na kampuni ya udalali ya Yono kutokana na wateja kutofikia malipo yanayotakiwa.

Nyumba hizo zilizoshindikana kununuliwa leo ni zile zilizopo Mbweni pamoja ya Upanga jijini Dar es Salaam.

Mnada huo ambao umekuwa ukisimamiwa na kampuni ya Yono, umeahirishwa kutokana na sababu za wateja ambao walitaka kununua nyumba hiyo kushindwa kufika bei ambayo ilitakiwa kuuzwa.

Wateja ambao walitakiwa kununua nyumba hiyo walikwama kwenye bei ya shilingi milioni 650 pekee.

Wakati huo huo katika nyumba ya kwanza iliyopo katika eneo la Mbweni JKT ilishindwa kununuliwa kutokana na tatizo kama hilo baada ya wanunuzi wa mwisho walikwama kwenye bei ya shilingi milioni 510.

Mnada huo unatarajia kufanyika tena hapo baadae utakapopangwa tena baada ya leo kushindikana kununuliwa nyumba hizo.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *