Baada ya zoezi la bomoabomoa kwa wakazi wanaoishi pembezoni mwa Barabara ya Morogoro katika maeneo ya Kimara na Mbezi jijini Dar es Salaam, zoezi hilo halikumuacha salama mbunge wa Mikumi na mwanamuziki wa Bongo Fleva, Profesa Jay.

Nyumba ya Profesa Jay ni miongoni mwa nyumba zilizowekwa alama ya X kwa ajili ya kubomolewa kupisha ujenzi wa utanuzi wa Barabara ya Morogoro.

Nyumba ya kifahari ya Profesa Jay si pekee itakayobomolewa kwani kuna nyumba nyingine ambazo zipo ndani ya mita 60 ambalo ni eneo la hifadhi ya barabara zitakazobomolewa na nyingine tayari zimebomolewa.

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) tayari limekata umeme kwenye baadhi ya nyumba zitakazobomolewa ili kupisha majanga wakati wa zoezi la ubomoaji.

Wananchi wa meneo hayo wameitaka serikali kuzungumza nao kabla ya kuendesha zoezi hilo la ubomoaji kwani wamejenga nyumba hizo kwa kujikongoja sana hivyo kuzibomoa kwa siku moja inawatia uchungu sana.

 

 

 

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *