Nyumba ya Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, Dkt. Amini Uronu imechomwa moto usiku wa kuamkia leo na watu wasiojulikana.
Mtoto wa Mwenyekiti huyo amesema kuwa Wazazi wake wote wamelazwa baada ya kapata madhara kiasi katika miili yao.
watu hao walichoma moto huo majira ya usiku wakati mwenyekiti huyo na familia yake walikuwa wamelala.
Jeshi la Polisi wilayani humo linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini waliotekeleza kitendo hicho cha kinyama kwa mwenyekiti huyo.