Nyumba ya mwanamuziki wa Uganda ambaye sasa ni mbunge Bobi Wine zimeshambuliwa na bomu na watu wasiojulikana.
Polisi sasa wanachunuza mashambulizi kwenye nyumba za Bobi Wine ambaye jina lake kamili anayewakilisha eneo la Kyaddondo West na Allan Ssewanya ambaye ni mbunge wa Makindye West.
Wiki iliyopita shambulizi liliripotiwa kwenye nyumba na mbunge mwingine Moses Kasibante ambaye ni mbunge wa Rubaga North.
Kwenye ujumbe kupitia mtandao wa Facebook, Bobi Wine alisema kuwa hakuna mtu aliyejeruhiwa nyumbani kwake
Wabunge ambao nyumba zao zilishambuliwa ni badhi ya wale waliotimuliwa bungeni kufuatia ghasia wakati wa mijadala kuhusu kuondolewa kwa umri wa kuwania urais.