Mwanamuziki wa rap Bongo, Rosa Ree amefunguka na kusema kuwa  nyimbo zake zote zilizokuwepo kwenye chaneli ya Youtube ya Industry zimefutwa.

Kipindi msanii huyo yupo chini ya label ya The Industry ngoma zake kama One Time, Up In The Air zilipatikana katika channel ya YouTube ya label hiyo lakini tangu aondoke The Industry channel hiyo imefutwa.

Rosa Ree amesema kuwa anafahamu toka mwanzo ila hajaamua kukipa nafasi kwa sasa katika muziki wake bali ameamua kujikita katika kutengeneza kazi nyingine mpya na zenye ubora.

Pia ameongeza kuwa The Industry wana haki zote kufanya hivyo kwani nyimbo hizo wao ndio wanazimiliki kisheria. Rosa Ree kwa sasa anafanya vizuri na ngoma ‘Marathon’.

The Industry ni label ambayo ipo chini ya kundi la Navy Kenzo, Label hii ilianza rasmi May, 2016 ikiwa na wasanii watatu, Wildad, Selina na Rosa Ree ila wote hawapo hapo kwa sasa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *