Nyangumi 400 wamekwama kwenye ufukwe wa bahari nchini New Zealand baada ya kushindwa kurudia baharini.

Nyangumi 300 wamekufa usiku katika ufuo wa Farewell Spit, katika kisiwa cha Kusini, katika kisa ambacho kinatajwa kuwa kibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo.

Mamia ya raia wa kujitolea wakisaidiana na maafisa wa uhifadhi wa wanyama na mazingira wamefanya juhuzi za kusaidia kuwarejesha nyangumi hao baharini.

Wanasayansi kufikia sasa bado hawajafanikiwa kufahamu ni kwa nini nyangumi hufika kwenye ufukwe wa bahari.

Lakini wakati mwingine inadhaniwa huwa inatokea kwa sababu nyangumi ni wazee sana au wanaugua, au wameumia, au wamepoteza mwelekeo hasa maeneo ambayo ufuo si laini.

Wakati mwingine, nyangumi anapokwama baharini, atawalilia wenzake ambao watafika kujaribu kumuokoa. Wengi mara nyingi nao hukwama maji yanapokupwa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *