Aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu amewashukuru Watanzania waliomsapoti wakati wa kukihama Chama Cha Mapinduzi.

Nyalandu amesema kuwa hoja zilizopo mbele kwa sasa ni kubwa kuliko mtu mmoja mmoja na zinalenga kuleta utashi kwa kila Mtanzania kutafakari na kushiriki kikamilifu katika safari ya kuendeleza nchi katika Demokrasia, uchumi na kijamii.

Nyarandu ametoa shukrani hizo kupitia mtandao wa kijamii na kuwaeleza watanzania jinsi gani wamemsapoti kutokana na uamuzi wake.

Mbali na hilo Lazaro Nyalandu amekanusha taarifa inayosambazwa ikionyesha kuwa alikuwa ana chat kupitia kundi la Whatsapp na baadhi ya viongozi wa CHADEMA akiomba akionyesha kuwa alifanya madhambi wakati akiwa Waziri wa Maliasili na kusema huo ni uzushi wa kutungwa na kusema ni siasa za kizamani hizo.

Nyalandu siku ya Jumatatu amejitangaza kukihama Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuomba kujiunga na Chama Cha Demokrasia na Maendelea (CHADEMA) ambapo viongozi wa chama hicho wamemkaribisha kujiunga nao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *