Mbunge wa Singida Kaskazini (CCM) Lazaro Nyalandu amesema kuwa kitendo cha askari kumuoneshea bastola aliyekuwa waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye kimedhalilisha taifa.

Kupitia akaunti yake ya Twitter Mbunge huyo ameanidka maneno ambayo yameonesha kusikitishwa kwake kutokana na matukio yanayotokea hapa nchini.

Kupitia twitter mbunge huyo ameandika,”IMESIKITISHA sana kuona AFISA akimtishia silaha Waziri Mstaafu Nape.Kitendo hicho ni kinyume na maadili ya TAIFA letu na kimedhalilisha NCHI,”

Pia ameongeza, “Kupitia BUNGE, nitaiomba SERIKALI ichukue HATUA za kinidhamu na kisheria DHIDI ya AFISA aliyemtishia Mh NAPE kwa SILAHA.Kitendo HAKIKUBALIKI,”

Katika sakata la RC Makonda kuvamia kituo cha Clouds Media alitweet, Katika kutekeleza wajibu wake KIKATIBA, BUNGE ni sharti lijadili na kutoa AZIMIO kuhusu kilichojiri CLOUDS FM, na UHURU wa VYOMBO vya HABARI,”

Mbali na mbunge huyo pia Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba amesema askari huyo aliyemuoneshea bastola Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye atachukuliwa hatua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *