Aliyekuwa mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu amejiunga rasmi na Chama cha Chadema baada ya kukabidhiwa kadi ya chama hicho jana.

Kadi hiyo ya Chadema amekabidhiwa jana na mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Freman Mbowe kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mhandu katika kampeni za uchaguzi mdogo wa udiwani.

Baada ya kukabidhiwa kadi hiyo Nyalandu amesema kuwa anashuru kupokelewa vizuri ndani ya Chadema baada ya kujiuzulu nafasi zake zote ndani ya CCM Oktoba 30 mwaka huu.

Nyalandu amesema kuwa alisubili kwa shauku kubwa siku hiyo ili apate fursa ya kujiunga na harakati za kupigania mageuzi ya kisiasa, mageuzi ya kijamii, mageuzi ya kiuchumi.

Pia Nyalandu alisema kuwa katika miaka miwili ya uongozi wa Awamu ta Tano ameaminia na kujiridhisha kuwa Chama cha Mapinduzi CCM kimepoteza mwelekeo wake ndiyo mana ameamua kuhama ndani ya chama hicho.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *