Mkali wa ‘Jike Shupa’ Nuh Mziwanda amesema kuwa anatamani mkewe Nawal ajiufungue watoto mapacha baada ya kupata ujauzito.

 Nuh Mziwanda amesema kuwa anakesha kila siku akimuomba Mungu amjaalie mke wake Nawal ambaye sasa ana mimba ya takriban miezi minne ajifungue watoto mapacha.

Pia Nuh amesema kuitwa baba wawili imekuwa ni ndoto yake ya muda mrefu na anaomba itimie kwa mkewe huyo kipenzi.

Naamini furaha yangu itakuwa zaidi ikiwa hivyo lakini hata akiwa mmoja pia nitashukuru. Kikubwa naomba mke wangu ajifungue salama ili na sisi tuingie kwenye ulimwengu wa wazazi,” alisema Nuh.

Wawili hao walifunga ndoa mwishoni mwa mwaka jana baada ya Nuh kuachana na Shilole.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *