Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amekanusha taarifa kuwa Shilole amevunja ndoa yake huku akidai wazazi wa binti huyo ndiyo chanzo.
Nuh ametoa kauli hiyo baada ya watu kudai kuwa kuvunjika kwa ndoa hiyo na mzazi mwenzie chanzo chake ni Shilole.
Mwanamuziki huyo ameendelea kusema kuwa “Unajua watanzania ukiwapa picha tu, basi wao wataandika maneno wataandika wenyewe Shilole hausiki hata kidogo kuvunjika kwa mahusiano yangu.”
Pia amengeza kwa kusema kuwa “Wahusika ni wazazi wake ambae yeye aliamua kuwasikiliza wazazi wake kwa kuolewa na mtu mwingine na hatukuwa na ugomvi wowote ila ndio hivyo wazazi walikuwa na nguvu sana kunizidi mimi,”.
Nuh Mziwanda aliongeza kuwa mahusiano yake ameyaweka kando na yupo kupambana na hali yake, lakini anashukuru Mungu mtoto wake bado anaendelea vizuri na anapata taarifa zote muhimu kumuhusu mtoto wake lakini mengine imebaki stori.