Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda amekanusha habari zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuwa amerudiana na aliyekuwa mpenzi wake Shilole.

Shilole na Nuh waliachana kipindi cha hapo nyuma ambapo baada ya kuachana waliingia katika vita ya kurushiana maneno mtandaoni.

Baada ya kuachana kila mmoja aliendelea na maisha yake binafsi huku Shilole huku Nuh akifunga ndoa na mrembo anayekwenda kwa jina la Nawal lakini baadae walikuja kuachana na Nawal kuolewa na mwanaume mwingine.

Nuh Mziwanda amesema kuwa hawezi kurudiana na Shilole tena bali anawatakia maisha mema yeye na mumewe Uchebe kwani penzi lao ni zilipendwa.

 Pia amedai kuwa zile picha zilizosambazwa mtandaoni wakiwa wamelala kimahaba zilikuwa ni picha ya siku nyingi sana wakiwa wapenzi na sio yeye aliyezisambaza kama Shilole alivyomtuhumu kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya Jana.

Kwa upande mwingine Nuh alifunguka na kudai kuwa tetesi za Kuwa amerudiana na mama wa mtoto wake, Nawal sio za kweli bali wanapatana kwa sasa kwa ajili ya kumlea binti yao na sio mambo mengine ya kimapenzi amedai kwa sasa hana mpenzi yoyote.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *