Aliyekuwa mpenzi wa zamani wa Shilole, Nuh Mziwanda amefunguka kuzungumzia mistari ya wimbo wa Mwana FA, ‘Bado Nipo Nipo’ aliyoipost muda mchache baada ya aliyekuwa mpenzi wake huyo wa zamani kuolewa na kijana anayetambulika kwa jina na Uchebe.

Baada ya Shilole kuolewa Nuh aliandika “Aliyelala na bibi harusi wiki moja kabla ya harusi na wala sio bwana harusi bado mnanishauri harusi’ kauli ambayo ilitafsiriwa na wadau wa mambo kwamba dongo hilo linaenda kwa Shilole na Uchebe.

Nuh amesema kuwa aliweka posti hiyo kwasababu ni msemo ambao nimeupenda na sipangiwi cha kukiposti na nimeandika si kwa ubaya na sijamtagi mtu hivyo nisinukuliwe vibaya coz niliandika na wala sikufikiria watu wangeusisha na harusi ya shilole ila ninavyojua hivi vitu vipo vinatokea kwa watu unamkuta bibi harusi kesho no harusi yake na analala na mwanamume mwingine.

Mimi na Shilole toka tuachane hatujawahi kurudiana ila uwa tunasaidiana pale inapoitajika kama kafiwa siwezi kuacha kwenda kumfariji kwakuwa tumeachana haipo hivyo na hata ngoma yangu ya sasa kuna baadhi ya vitu amenisaidia kuingiza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *