Mwanamuziki wa hip hop Bongo kutoka kundi la Weusi, Nikki wa Pili amefunguka na sababu ya muziki wa hip hop kukosa verse tatu.
Nikki wa Pili amesema kuwa muziki unaendana na mapokeo yake na media nyingi sasa zinapiga muziki verse moja au mbili, pia wasanii wa Bongo Flava hawataki kukumbwa na kitu kilichokumba muziki wa band au taarab kutoka na nyimbo zao kuwa refu.
Mwanamuziki huyo amesema kuwa “Kwa hiyo watu wa media sasa hivi time zao ni ndogo, wanahitaji nyimbo fupi ili waweze kupiga muziki mwingi ili mtu anayesikiliza aone muziki unaenda ukibadilika, kwa hiyo sisi kama wasanii wa kizazi kipya tumeenda na time,”.
Pia amesema kuwa “Ukisema sasa unapiga verse tatu hamna mtu atasikiliza na kama unapiga inabidi iwe fupi, ndio maana ukisilikiza wimbo kama Dude au Madaraka ya Kulevya verse yangu ina mistari kama nane au 12 tu”.