Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nikki wa Pili amesema mwanaume kumsomesha mchumba ni kujiongezea baraka kwani binadamu wameumba katika kusaidia wengine.

Hayo ameyasema baada ya wiki iliyopita mchumba na mama wa mtoto wake kukiri kwamba yeye  (Nikki) ndiye aliyemlipia ada mbali na michango mingine kwenye safari yake ya kufikia alipofika.

Nikki amesema kwamba ukimsomesha mtu unatakiwa kujivunia mafanikio hayo kwani dini inafundisha kusaidia.

Nikki ambaye anajulikana zaidi kwenye kiwanda cha burudani akitokea kundi la Weusi, anasema wakati mwingine unatakiwa kutoa hata kama hutafaidi matunda kwani hata vitabu vya dini na jamii ndivyo inavyofundisha na kusisitiza hata kama mchumba ake huyo (Joan) wasingekua na mtoto bado angeweza kumsomesha

Akizungumzia kuhusu kufunga ndoa na mchumba wake huyo ambaye pia ni mama wa mtoto wake (Zuri) Nikki anasema mipango ipo japo mapenzi ni ya wawili, ikifika wakati wakakubaliana basi watafunga pingu za maisha.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *