Kiungo wa Ufaransa na Klabu ya Chelsea, N’Golo Kante ameshinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Mwaka wa Waandishi wa Habari za Michezo (FWA).

Kante alipigiwa kura kushinda tuzo hiyo akiwapiku mchezaji mwenzie wa Chelsea Eden Hazard na mchezaji wa Tottenham Dele Alli kwa zaidi ya 65% ya kura zote.

Kabla ya tuzo ya FWA tayari N’Golo Kante alitwaa tuzo ya PFA na sasa anakuwa mchezaji wa 20 kutwaa tuzo hizo mbili kwa pamoja.

Mwenyekiti wa FWA Patrick Barclay (kushoto) akimkabidhi N’golo Kante tuzo ya FWA.
Mwenyekiti wa FWA Patrick Barclay (kushoto) akimkabidhi N’golo Kante tuzo ya FWA.

Utoaji wa tuzo hiyo umefanyika Hoteli ya Landmark na kuhudhuriwa na watu kibao maarufu pamoja na wachezaji mpira wa zamani.

Kiungo huyo ameonyesha kiwango kibwa sana msimu huu mpaka kupelekea kuisadia timu yake ya Chelsea kutwa ubingwa wa Uingereza na kutinga fainali ya kombe la FA ambayo atakutana na Arsenal.

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *