Mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Neymar anatarajiwa kuwa fiti na kushiriki katika Kombe la Dunia msimu huu wa joto litakalofanyika nchini Urusi.
Mchezaji huyo anatarajiwa kurudi katika mazoezi Mei 17 baada ya kuwa nje kufuatia kuvunjika mguu.
Mchezaji huyo wa kiungo cha mbele wa Paris St-Germain alihitaji kufanyiwa upasuaji mfupa baada ya kujeruhiwa katika mechi ya ligimnamo Februari 25.
Brazil inacheza mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Switzerland Juni 17, mwezi mmoja baada ya muda anaotarajiwa kurudi uwanjani.
Neymar alikuwa mchezaji mwenye gharama ya juu wa soka alipojiunga na PSG kutoka Barcelona Agosti mwaka jana, na amefanikiwa kufungua magoli 25 huku akiwa amesaidia kufanikisha mara 16 kufunga kwa timu hiyo ya Ufaransa msimu huu.
“Nafanyiwa ukaguzi wa mwisho Mei 17 na baada ya hapo nitaweza kucheza,” ameambia mkutano wa waandishi habari mjini Sao Paulo, ambako amekuwa akipokea matibabu.
“Ninafanyiwa ukaguzi kila siku, na kuanzia nitakapo anza kufanya mazoezi nitatia bidiii zaidi ya nilivyokuwa nikijitahidi kwasababu hii ni ndoto inayokuja. Ni Kombe la Dunia. Nimesubiri miaka minne kwa nafasi hii, ipo karibu.”