Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar na klabu yake watasimama kizimbani kujibu mashtaka ya uhamisho wa mchezaji huyo, kutoka klabu ya Santos, baada ya kushindwa rufaa.
Kesi hiyo inaihusu kampuni ya uwekezaji ya Brazil DIS, inayomiliki asilimia 45 ya mauzo ya Neymar imelalamika kuwa ilipewa kiasi kidogo cha fedha, wakati Neymar alipouzwa Barcelona kutoka Santos, kwa ada ya £49 mwaka 2013.
Klabu ya Santos, Neymar, Mama yake na kampuni inayomilikwa na wazazi wake, watafikishwa mahakamani.
Neymar anaweza kukumbwa na kifungo cha miaka miwili jela na faini ya paundi milioni 8, endapo atapatikana na hatia.
Lakini kwa mujibu wa sheria za Hispania, kifungo chini ya miaka miwili hutolewa na kubaki faini peke yake.