Mshambuliaji wa Barcelona, Neymar Jr amefutiwa mashtaki ya madai yaliyokuwa yanamkabili na Mahakama ya rufaa nchini Brazil.
Hayo yamejili baada ya wakaguzi wa hesabu kushindwa kuthibitisha madai ya mchezaji huyo kutakiwa kulipa kodi ya mapato kiasi cha euro milioni 27.5 badala ya kiasi alicholipa.
Pia Mahakama hiyo imempa uhuru Neymar Jr kuruhusiwa kutumia picha zake za matangazo kusimamiwa na kampuni za familia yake.
Mwaka 2015, Neymar alishtakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi ya zaidi ya euro milioni 63 zilizotokana na mapato yake katika vilabu vya Santos na Barcelona na matangazo kati ya mwaka 2011 na 2014.
Neymar anapaswa kulipa nusu ya kiasi cha euro milioni 200 anachodaiwa na maafisa wa kodi hata kama atashindwa madai mengine yaliyobaki dhidi yake.