Mastaa wa HIP HOP hapa Bongo, rapa mtata Ney wa Mitego na legendary Profesa Jay wamepewa heshima maalum na Baraza la Sanaa Taifa (BASATA) kwa kuwa wasanii wanaotii sheria ya kuwataka kusikilizisha mashairi yao kabla ya kutoa ngoma.
BASATA imewataja mastaa hao kuwa vinara wa kupeleka ngoma zao kwenye taasisi hiyo huku wasanii wengine wakiangukia kwenye kufungiwa nyimbo zao kutokana na kukaidi utaratibu huo.
Ngoma ya rapa NIKKI MBISHI, I am sorry JK ilifungiwa siku za karibuni kutokana na kukiuka masharti ya kanuni hiyo.
Ngoma ya Ney wa Mitego, HAPO KATI nayo pia iliingia kwenye mkumbo wa kufungiwa na BASATA.
Je ngoma za mastaa wengine zinazotolewa bila kupitiwa hupewa hukumu gani kama mashairi yake yana mashairi yanayokubalika?