Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limeng’oa mitambo ya umwagiliaji iliyopo katika shamba mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na kumtoza faini ya milioni 18 kwa kuendesha kilimo eneo lisiloruhusiwa.

Mbowe amepigwa faini hizo kwa kosa la kuendesha shughuli za kilimo ndani ya eneo la mita 60 kutoka kilipo chanzo cha maji.

Baada ya tukio hilo kutokea, Mbowe amesema kuwa zoezi zima limeendeshwa kisiasa na hii kuthibitisha kuwa nchi yetu inaongozwa kwa chuki na husda kutokana na tukio hilo.

Mbowe alisema kuwa walipopewa taarifa mara ya kwanza, walikata rufaa kwa waziri husika kwa sababu sheria inaruhusu hivyo hadi sasa walikuwa wakisubiria majibu ya rufaa hiyo.

Baada ya tukio hilo, Mbowe alieleza kuwa atawasiliana na wanasheria wake ili kujua hatua zitakazofuata.

Zoezi hilo la kung’oa miundombinu kwenye shamba hilo la Kilimanjaro Veggies lilifanyika jana chini ya Mkuu wa Wilaya ya Hai, Gelasius Byakanwa na maofisa wa NEMC.

Shamba hilo la Mbowe liko katika Kijiji cha Nshara, Machame ambapo Januari 20 mwaka huu, DC Hai alifika shambani hapo na kusitisha shughuli zote za kilimo kutokana na eneo hilo kuwa ndani ya chanzo cha maji.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *