Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nedy Music amekanusha kutoka kimapenzi na mwanamuziki mwenzake Karen licha ya ukaribu wao.

Stori za wao kutoka kimapenzi zilianza baada ya Nedy Music kumpost mara kadhaa Mrembo huyo katika Ukurasa wake wa Instagram akisindikiza na Maneno kama ‘I LOVE YOU’.

Kutoka na kupostiana hivyo wengi wakapigia Mstari kuwa wawili hao Tayari wapo kwenye Mahusiano ya Kimapenzi na baadhi wakahisi hata Mtoto wa Amezaa na Staa huyo.

Karen kwa upande wake hakuongea chochote kuhusu tetesi za yeye kuhusishwa kutoka kimapenzi na mwanamuziki huyo kutoka visiwani Zanzibar.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *