Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema ataunda timu yake itakayofuatilia suala la madini ya almasi.

Ndugai ameyasema hayo leo baada ya kamati ya pili kutoa ripoti yake kuhusu mchanga wa madini katika makontena 277 yanayoshikiliwa.

Amesema kwa kushirikiana na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye ni kiongozi wa shughuli za bunge, watasaidiana kuunda timu hiyo ili kumsaidia Rais katika masuala ya madini.

Amesema kuwa ‘Kwa pamoja, rais ukienda huko na sisi tukienda huku, tutafika kufanikisha tatizo hilo la mchanga wa madini’

Tayari Spika alishaunda kamati kuchunguza suala la madini ya Tanzanite kabla ya kamati zilizoundwa na rais Magufuli kutoa ripoti.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *