Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wabunge watakaofanya vitendo vya utovu wa nidhamu bungeni hawatavumiliwa na huenda adhabu ikaongezeka maradufu kwa wasiozingatia kanuni.

Ndugai aliyekuwa nje ya nchi kwa mwezi mmoja akitembelea Nigeria, Dubai na Iran alisema hayo jana alipojibu swali la mwandishi wa habari.

Spika Ndugai alisema vikao vya mkutano ujao wa Bunge vitaanza Septemba 5. β€œTumekuwa tukiwatoa nje mara kadhaa lakini imefika mahali tumewafungia wengine mwaka mzima, ila sasa tumechoka wakirudi na wakaendelea na jeuri yao msishangae adhabu zikapanda na kuwa kubwa zaidi, kwa sababu tumechoka,” alisema.

Wabunge Halima Mdee (Kawe) na Ester Bulaya (Bunda Mjini), wote Chadema, walisimamishwa katika mkutano uliopita wa Bunge kuhudhuria vikao vya mkutano wa saba, nane na wa tisa hadi mwakani, ambapo watalipwa nusu mshahara na posho zinazoambatana nao kwa miezi 10 kwa mujibu wa kanuni ya 75 ya chombo hicho cha kutunga sheria.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *