Shirika la ndege la Malawi, Malawi Airlines limetangaza kufanya safari ya ndege itakayosimamiwa na wanawake pekee kuanzia kesho.

Safari hiyo ya ndege, ambayo itakuwa na marubani na wasaidizi wa abiria kwenye ndege wote wakiwa wanawake, itakuwa ya kwanza kuandaliwa na shirika hilo.

Ndege hiyo itasafirisha abiria kutoka mji wa Blantyre hadi Dar-es-Salaam nchini Tanzania na itatua kwa muda Lilongwe kabla ya kuelekea Dar .

Ndege hiyo itakuwa chini ya Kapteni Yolanda Kaunda akisaidiwa na Lusekelo Mwenifumbo.

Bi Mwenifumbo, 24, alisomea taaluma ya uchukuzi wa ndege mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *